Alama ni nini? Ni kielekezo au ishara ambayo inawekwa au inakuwepo kuweza kutambulisha kitu Fulani. Tumekuwa tukiona sehemu mbalimbali kwa wafanyakazi wa mahali fulania au wanafunzi wanakuwa wanapewa vitambulisho, hivi ni alama ambazo zinawafanya watambuliwe.
KUTOKA 12:7-13, 21
Utakumbuka wana waisraeli walipokuwa utumwani huko Misri, walipata shida kubwa sana, wakamlilia Mungu wao. Haikuwa rahisi kwao wana waisraeli kuweza kupewa kibali, na walipopewa kibali bado adui yao hakuchoka kuwafuatilia. Hivyo sisi kama wakristo tusifike sehemu tukaona Mungu ametusaidia halafu tukaamua kumsahau, tuwe na uhakika Zaidi kuwa kila baada ya kupata ushindi katika jaribu Fulani( vita ) , adui zetu huwa wanajipanga Zaidi ili kuja kutuangusha, ndivyo ilivyokuwa kwa wana waisraeli, Farao aliyekuwa mfame wa ‘[Misri alipokataa kuwapatia ruhusa wana waisreli, Mungu aliamua kuachilia mapigo kumi (10) ,pigo la mwisho ni lile la kufa kwa wazaliwa wote wa kwanza wa Misri huku wana waisreli wakiwa salama kabisa. Unaona damu ya mwana kondoo ambavyo inatumiwa kama alama ya kuweza kutuepushia kila aina ya taabu kubwa au kuwa kinga kubwa katika maisha yetu.
Unajua kama wasingeweka damu katika milango yao, pia wao wangeweza kupatwa na vifo sawa na vile vilivyowapata wamisri? Unajua mtu wa Mungu, Mungu anavyokwambia fanya hivi, jitahidi kufanya hivyo, maana kwa kufanya hivyo unakuwa unajiwekea alama ambayo itamfanya Mungu wakati akiwa anapita kubariki watu wake asije akakusahau au wakati akiwa anaangamiza asikuangamize. Na wana waisraeli waliambiwa wakae ndani ya nyumba zao, wala wasijetoka nje ambapo wakati wa usiku wa manane Malaika wa uangamivu atakapokuwa akipita asiweze kuwaangamiza.
Baada ya Farao kuwapa ruhusa kwamba waondoke, bado aliwafuatilia tena kuhakikisha kuwa hawaondoki. Ndivyo unapoona umewashinda adui zako, usiwe ni wakati wa kubweteka na kuridhika, huo ndiyo wakati mzuri wa kumtafuta Mungu ili aonekane Zaidi katika maisha yako. Watu wengi wamekuwa wakikutana na shida wanamkumbuka Mungu, lakini baada ya shida zao kuisha wanamsahau Mungu, wanashindwa kujua tayari wametangaza vita na adui, halafu wanakimbilia maeneo yasiyokuwa salama(yasiyokuwa na ulinzi).
Wana waisraeli walipata taabu njiani lakini kubwa kuliko huwa ni pale walipofika mwisho wa njia yao( walipofika katika bahari ya shamu). Lakini kwa kuwa hawakuianzisha safari wao wenyewe kwa akili zao bali Mungu mwenyewe aliianzisha safari ndiye alikuwa anajua kuwa atawafikisha huko waendako. Unajua Mungu wakati mwingine anakuwa ametuonyesha twende sehemu Fulani, lakini inafika sehemu anaamua kutupitisha mahali Fulani ambapo akili yetu inakuwa imekoma ili tu atutazame, kwamba hivi tunaamini kuwa tutasonga mbele katika shida hiyo? Suala la tutapitaje katika shida hii huwa si kazi yetu, kazi yetu ni moja tu, kuwa tumwambie Yesu kuwa tumefika kwenye kizingiti hivyo tunahitaji afanye njia.
Wana waisreli walipovuka ile bahari ya shamu, haikuwa mwisho wa majaribu yao, bali ulikuwa kama ndiyo mwanzo wa majaribu yao.
YOSHUA 2:18
Wana waisraeli walipovuka mto Yordani, mtumishi wa Mungu Yoshua alichagua watu wawili waliokwenda kuupeleleza mji wa Yeriko, na haikuwa kazi nyepesi kama ambavyo wengi wanafikiri na kudhani. Maana Yeriko ulikuwa mjia ambao ulikuwa umejengwa na kuzungukwa na ukuta mkubwa na kuwa na sehemu maalumu kwaajili ya kuingilia na kutokea. Kama ambavyo miji mingi ilivyokuwa katika Afrika na sehemu zingine nyingi hapa duuniani, miji ilikuwa inazungushiwa na kuta nene kwaajili ya ulinzi na sababu zingine za usalama. Tunawaona hawa watu wawili waliotumwa kwenda kuipeleleza Yeriko, wanaingia ndani ya Yeriko kupitia lango kuu sawa sawa na wageni wengine au wasafiri wengine. Wao walikuwa wageni , na wakaenda mahali ambapo wageni wengine wangekwenda kwa kawaida, aina Fulani ya hoteli au nyumba ya kulala wageni ambayo ilikuwa imejengwa juu ya mkao wa ukuta ule. Mwanamke alikuwa ndiye mwenye hoteli hiyo na alikuwa kahaba pia. Isingeonekana kuwa kitu cha ajabu kwa watu hao kwenda mahali kama hapo, maana hii ilikuwa ni desturi ya watu wasiomcha Mungu, hata kama ilivyo mpaka leo hii.
Lakini watu wengine waliwaona wale wapelelezi na kufahamu kuwa ya kuwa walikuwa wageni. Kwahiyo mfalme akapewa taarifa za ujio na uwepo wa wageni hao, na akaamua kutuma askari ili kuwa kamata watu hao wawili. Na uwe na uhakika kabisa kuwa kipindi hicho pia kulikuwa na kusambaa kwa taarifa mbalimbali hasa za kivita kati ya falme mbali mbali, hivyo Yeriko walifahamu kwamba waisreli walikuwa karibu sana , upande wa pili wa mto. Na kutokana na yale ambayo yule mwanamke kahaba alisema baadaye, watu vilevile walikuwa wamekwisha kusikia kuhusu ule ushindi wa ajabu na wa namna yake ambao Mungu alikuwa amewafanyia wana waisraeli. Lakini yule mwanamke kahaba alikuwa na Imani na kufikiri moyoni mwake kuwa hawa watu kweli wametoka kwa Mungu.
Tunamuona huyu mwanamke kahaba alikuwa na sifa mbaya sana;
Kwanza alikuwa ni kahaba
Pili alikuwa muongo
Na Biblia iko wazi kabisa na imetaja haya yote, na Neno la Mungu haliungi mkono dhambi ya aina yeyote katika mazingira yeyote. Dhambi ni dhambi tu, haijalishi imetendwa katika mazingira yepi au katika wakati gani au kwa madhumuni gani, bado Neno la Mungu litasimama palepale. Agano la kale lilikuwa na sharia kali dhidi ya matendo machafu ikiwemo uongo ( Walawi 19:11), lakini utakumbuka Rahabu alikuwa mwanamke au mtu wa mataifa, kwahiyo alikuwa mpagani. Dini yake haikuwa na masharti kwaajili ya kuishi maisha matakatifu. Yeye alikuwa anafanya kile kilichokuwa desturi kwake. Lakini Mungu aliona ndani sana ya moyo wake, shauku ya kutaka kuijua njia ya kweli na yenye uzima wa milele. Ni kweli kabisa kuwa hatuwezi kutazamia mwenye dhambi kuwa mwenye haki kabla hajaokoka, wakati mwingine hatuwatii moyo watu hawa waovu kwenda kanisani kwa vile tuna hofu kwamba hawatampendeza Mungu, nawakati mwingine watu watatutazama vipi sisi wakutuona tukiwa na hawa watu. Lakini mkumbuke Yesu mwenyewe(LUKA 5:31), lipokuwa akiwajibu wale Mafarisayo, kwamba wasio wagonjwa hawahitaji tabibu. Kwa hiyo kukaa na watu hawa kwaajili ya lengo la kuwasaidia kiroho siyo jambo baya. Tuwalete makanisani na wlisikie Neno la Mungu kasha watatubu na kubadilika. Biblia na Neno la Mungu haliungi kono matendo ya Rahabu hata kidogo. Rahabu aliwaambia wale wapelelezi kwamba yeyey alikuwa anaamini kwamba Mungu wa Israeli angewapa nchi ile. Kwa kweli watu wote wa Yeriko walikuwa na hofu sana. Maana walikuwa wamesikia kuhusu jinsi ambavyo Mungu alikuwa amewatengenezea njia katikati ya bahari, na kuwavusha mto Yordani, pia jinsi Mungu alivyowapa ushindi juu ya Sihoni na Ogu. Rahabu naye alikuwa amesikia habari za wana waisreli kuhusu uweza na mkono wa Mungu ambavyo ulikuwa ukijidhihirisha juu yao.
Pamoja na hofu kubwa aliyokuwa nayo Rahabu, bado alikuwa tayari kumpa maisha Mungu wa Israeli, dini yake yeye mwenyewe isingetosha , japo alikuwa dini hiyo ilikuwa na miungu wengi tu, lakini Mungu huyu wa Israeli alikuwa mkuu sana na Zaidi ya miungu mingine. Yeye alikiri hivyo, na hilo ndilo lililomletea wokovu wake. Watu wengine katika Yeriko walikuwa na ufahamu huo huo lakini hawakutaka kumkiri na kumgeukia Mungu wa Israeli na hawakuhitaji msaada wake. Wowote wale ambao wangemkiri Mungu wa Israeli wangeokolewa.
Rahabu aliwaomba wapelelezi wamhurumie kama malipo kwaajili ya kuwahifadhi, na wle wapelelezi waliahidi kuwa angeokolewa wakati ambapo Mungu anewapa mji huo wa Yeriko. Yeye aliwasaidia sana, aliwapitisha dirishani kwa njia ya kamba , wakatokea nje ya ule ukuta na wakaenda zao salama. Watu wale walimpa Uzi au kamba nyekundu ili aitundike kwenyedirisha lilelile. Hii ingekuwa ni ALAMA kwao kwamba mtu yeyote ambaye alikuwa katika nyumba ile angeokolewa kama majeshi ya Israeli yangekwenda kuupiga mji wa Yeriko. Lakini Rahabu na jamaa yake wangekuwa salama kama wangebakia katika ile nyumba yake iliyo na uzi au kamba nyekundu. Hivyo kama ingetokea Rahabu akatoka nje ya nyumba yake ambayo ilikuwa na uzi mwekundu lazima naye angeuawa.
Huu uzi mwekundu unazungumzia kuhusu wokovu wa Mungu kupitia damu ya Yesu kristo wa Nazareti. Israeli walikuwa wameokolewa katika misri kwa kutia damu au kuipaka juu ya miimo ya milango wakati malaika wa kifo alipopita katika nchi ya kukaa kwao. Leo sisi tunaokolewa kwa damu ya yesu , na hakuna wokovu katika chochote kingine. Sisi tunaokolewa wakati tunapobakia chini ya ulinzi wa damu. Ikiwa tutaondoka humo na kwenda kuangalia ulimwengu wa dhambi , basi hatuna ulinzi huo tena. Wale wapelelezi wawili walijificha wao wenyewe katika mawe walipopata nafasi ya kurudi kwa watu wao. Huko watatoa taarifa kwa Yoshua kwamba Mungu alikuwa amekwisha kuwapa mji huo. Hii ilikuwa ni kwa Imani tu!
Mungu akubariki sana.
LOVE OF CHRIST TO ALL NATIONS(LoCN) is a Ministry that is Committed to Preach the Word of God, as this is what Jesus Ordered to his Disciples. This is Fundamentals for all Christians, and this is his wishes, that everyone hears his word, as preachers and Missionaries we're really committed to achieve this Goal, and if you wish to join us let you be blessed and pray for us.
YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!

- A SALVATION TO ALL NATIONS (ASANA)
- We're delightly to preach the word of almighty God
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment