Bwana YESU asifiwe sana watu wa Mungu!
Naitwa Ev Dr. Ayubu Mathias Kwandikwa, kutoka chuo kikuu cha Askofu mkuu Yakobo (Archbishop Jamaes university College) chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Agustino, nimeokoka na ninampenda Yesu na ninamtumikia katika kazi yake kwenye eneo la uijnilisti..
Ninaunga mkono jitihada za serikali katika kupamba na suala la uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, niwapongeze viongozi mbalimbali ambao wameamua kwa dhati kabisa kutaka kulitokomeza suala hili.
Lakini kipo kitu kimoja ambacho serikali ningependa niwashauri, hakuna kitu kizuri kama kuanza na Mungu halafu ukamaliza na Mungu; Hatuwezi kufanikiwa vita hii kama watu hawajamjua Yesu kristo, unajua mtu akiokoka Anabadilishwa, anafanywa kuwa upya, matendo yote ambayo alikuwa nayo yasiyompendeza Mungu ni lazima yaachwe ili mtu awe amebadilika.
Lakini kama hatuwezi kumshirikisha Mungu hatuwezi pia kufanikiwa, na ndio maana anasema katika kitabu chake kitakatifu cha Biblia anasema "BWANA ASIPOULINDA MJI WAKESHAO WAKESHA BURE".
Na ndiyo maana tunaona mataifa mengi yamefanya vita dhidi ya madawa ya kulevya lakini bado wameshindwa, sasa uwe na uhakika pia kwetu kama tutaifanya hii vita bila kumshirikisha Mungu tutashindwa.
Madawa ya kulevya si kitu cha mchezo maana yana madhara makubwa kwa mtumiaji, familia yake, na hata jamii na taifa kwa ujumla.
Nawaasa vijana wote kujiepusha na uuzaji,utumiaji au kuwa katika mitandao ya aina yeyote inayohusu madawa ya kulevya.
Mungu awabariki sana.
Mawasiliano: ayubumathi@gmail.com
LOVE OF CHRIST TO ALL NATIONS(LoCN) is a Ministry that is Committed to Preach the Word of God, as this is what Jesus Ordered to his Disciples. This is Fundamentals for all Christians, and this is his wishes, that everyone hears his word, as preachers and Missionaries we're really committed to achieve this Goal, and if you wish to join us let you be blessed and pray for us.
YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!
- A SALVATION TO ALL NATIONS (ASANA)
- We're delightly to preach the word of almighty God
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ukizingatuz waathirika wakubwa ni vijana nguvu kazi ya taifa
ReplyDeleteTunatakiwa kukemea kwa nguvu zote
Eeh mungu tuongoze