AINA YA KWANZA
I. HISTORIA YA MTU KABLA YA KUMFAHAMU YESU KRISTO NA KUMPOKEA KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE:
Hii inakuwa ni ile historia anayokuwa nayo kila mtu. Hii ni lazima utaipitia tu, na ni kwa sababu hakuna aliyezaliwa akiwa amemuamini Yesu Kristo kuwa ni BWANA na mwokozi wa maisha yake. Na hapa bado watu wengi hawajafahamu kuwa ukizaliwa katika familia ya kikristo haina maana kwamba tayari umempokea Yesu Kristo na kumkubali kuwa ndiye mwokozi wa maisha yako. Kumpokea ni sehemu ya kwanza lakini pia kumkubali kuwa ndiye BWANA na mwokozi wa maisha yako ni sehemu ya pili. Na Biblia imeweka bayana kabisa kwa habari ya kumfuata na kumkubali Yesu (Luka 12:8-9), haina sababu ya kuendelea kuwa unadhani uko upande Fulani lakini kumbe hauko upande huo,sasa ni muhimu sana kuwa makini kwa hili. Kumfuata Yesu ni lazima ujikane mwenyewe, siyo suala la kukuta wazazi wako wana Sali, na wewe ukaamini kuwa tayari haina haja ya kuokoka (yaani kumkiri Yesu kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako, yaani uokoke kwa kumkiri kwa maneno ya kinywa chako). Kati ya vitu ambavyo vimenisumbua katika maisha yangu ni kuhusu kuokoka huku tayari nilikuwa ni kisimama majukwaani kwenye mikutano na kuhubiri, nimesimama kwenye madhabahu na kuhudumu, lakini bado nikawa sina Amani.
Roho yangu ilikosa Amani kwa sababu nimezaliwa katika familia ya kikristo na kukulia katika familia ya kikristo, lakini bado nilidhani kuwa haina haja ya kuokoka maana ukizaliwa katika familia ya kikristo tayari utakuwa umeokoka, lakini sikweli, ni lazima umkiri Yesu kwa kinywa chako mwenyewe (Warumi 10:9-11), hivyo huwezi okolewa wala kuwa katika ufalme wa Mungu kama hujamkiri kwa kinywa chako wewe mwenyewe. Mungu akujalie kuelewa ujumbe huu, jitahidi uelewe kitu gani Mungu anakihitaji kwako wewe mwanadamu aliyekufilia pale msalabani.
Ikawa siku moja Roho wa BWANA akawa ananisihi niokoke, lakini maswali makubwa yaliyokuwa kichwani mwangu ni; hivi kweli sijaokoka? Hivi watu watanichukuliaje? Si nitazua maada vichwani kwa watu kwamba alikuwa anasimama kuhubiri, leo imekuwaje? Au katenda dhambi jana?Lakini kile nilichokifanya ni kulitazama neno la Mungu linasemaje, nakumbuka ilikuwa ni kwenye semina katika kanisa moja lililoko mkoani Ruvuma, ndipo aliposimama mama mmoja kufundisha katika ile semina, na ndipo somo alilotufundisha likawa na majibu ya kile kilichonisumbua siku nyingi, ndipo nilipoamua mwenyewe kuokoka.
Baada nikawa na amani moyoni mwangu. Yesu anawambia wanafunzi wake kuwa anayetaka kunifuata lazima ajikane yeye mwenyewe (Luka 9:23), maana yake uamue wewe mwenyewe bila kufanya hivyo kwa sababu pengine umezaliwa ukakuta ni kama desturi kwenda kanisani na leo unatembea na kusema umeokoka, lakini kumbuka Yesu mwenyewe anasema kila mtu atakaye mkiri mbele ya watu, hata yeye atamkiri mbele ya Baba yake aliye mbinguni (Mathayo 10:32). Na bahati mbaya wengine tayari ni viongozi, ni watu wa kubwa wana majina yenye sifa na hivyo wanaogopa kukiri na kujishusha, (Yohana 12:42). Usiogope eti watu watakutenga, ni bora wakutenge lakini uurithi ufalme wa Mungu, kwani utapata faida gani endapo wanadamu watakuona umeokoka lakini kumbe Mungu hakutambui?.Ule wakati wa kukata kauri unafika ambapo hatima ya kila mtu itajulikana kuwa ulikuwa wa Mungu au laa! Ionekane kuwa kumbe mhubiri ulikuwa hujaokoka?, mchungaji ulikuwa hujaokoka? Muimbaji ulikuwa hujaokoka? Inauma sana, maana unautumia muda wako kumtumikia Mungu lakini hakutambui.
Historia tunayo zaliwa nayo kwa kawaida ndiyo inayoendelea kutujengea kesho yetu sisi, sasa usipokuwa makini itakuwa ni shida sana. Ni kweli yamkini hukuzaliwa katika familia ya kikristo , lakini umeishi maisha ambayo hayampendezi Mungu, bado ipo nafasi ya kuweza kurekebisha nafasi hiyo na kuibadilisha historia yako, watu walizoea kukuona wewe ni mzinzi lakini leo acha huo uzinzi, watu walizoea kukuona ukitukana, ukilewa pombe,ukitoa matusi, ukifanya udharirishaji, ukiiba, ukisaliti, ukifanya mambo yasiyo mpendeza Mungu, achana yano, njoo kwa Yesu.Yesu anakupenda sana ndiyo maana umepata nafasi nyiningine hii hata yakuweza kusoma ujumbe huu.
Mfano mzuri ni Mtume Paulo (aliyekuwa Sauli hapo awali) Matendo 8:1- . Alikuwa mtu ambaye anaogopeka sana kwa sababu alikuwa akiwaua watumishi wa Mungu, katika kipindi hiki, ni kipindi ambacho kinakumbukwa sana kwa maana ni kipindi ambacho kanisa lilipata wakati mgumu, Amani ilitoweka, waumini wa kanisa pia walipata wakati mgumu. Lakini kwao mitume ilikuwa ni tofauti kabisa maana kabla ya kipindi hiki Yesu alijua wakati huu mgumu ambao kanisa linakwenda kuupitia na ndiyo maana alisisitiza mitume wajazwe na Roho mtakatifu, maana bila ya Roho mtakatifu wasingeweza kustahimiri mateso ambayo yaliwakabili katika kipindi hicho. Sauli alitumika kutimiza kusudi la kipindi kile, aliwaua mitume wengi sana, ikafika kipindi akawa anaogopeka sana hata anapoonekana mtaani hata kama hana mpango wa kufanya mauaji, kwake alikuwa akijisikia viziri sana kufanya vile, wakuu wa sharia walimtumia sana maana hakuwahi kushindwa kufanya kitu ambacho walikuwa wakimuagiza afanye. Hivyo alijikuta anaogopeka sana,na historia yake ikajengeka kuwa huyu mtu siyo wa kawaida hata kidogo, kwa hali ya kawaida Sauli alikuwa siyo mtu wa kawaida maana tabia na mwenendo wake vilikuwa vinatisha, na hata mitume walipomuona Sauli walikuwa wanatambua kuwa yamkini leo ni mwisho wao. Historia yake ikajengwa katika misingi ya kuogofya, akawa ni mtu anyeogopeka kila mahali kwa sababu ya matendo yake hayo.
Lakini nataka nikwambie kitu kimoja ndugu yangu, ni bora wanadamu wakuone hufai na hunathaamani lakini ukampata Yesu, yeye ni wathamani. Haohao ambao wanakushangaa na kukuona hufai na wakikuona ukifanya vile wanavyotaka ndiyo wanafurahi, kumbuka wao pia ni wanadamu, ipo siku watakufa (Ayubu 14:1-2). Yesu yeye yupo milele yote, anasema yeye ni yule yule jana na leo na hata milele, ukiwa na Yesu hatakuacha katika shida yako, yeye hatakufa, kwahiyo ukimtegemea yeye inakuwa ni bora sana kwa sababu yeye hafi yupo milele yote.
Wengine wanaogopa kuokoka kwa sababu wanajua wameishi maisha yasiyompendeza Mungu hata wanadamu, hivyo wanaona kwamba hivi wanadamu wataamini kuwa kweli tumeokoka na kuacha dhambi zetu? Nataka nikwambie kuwa hauokoki ili kumfanya jirani yako, mzazi wako, rafiki yako au mwanadamu yeyote ajue kuwa umeokoka! Bali unaamua kuokoka ili kuyaponya maisha yako, haina maana ya kuwasikiliza wanadamu huku wanadamu hawana mbingu yeyote ya kukupeleka. Usiogope wanadamu wanasema nini, bali tazama kuwa maisha ya hapa duniani yanapita, iko sehemu Mungu ameiandaa kwaajili yako. Usiwaogope wanadamu kwa sababu ukiwaogopa wanadamu ukakataa kumkiri Yesu ile mbingu siyo kwaajili yako (Luka 9:26), usiwaangalie marafiki, ndugu zako au wazazi wako wanasema nini kwa sababu siku ile ya mwisho utasimama wewe kama wewe ili utoe hesabu yako, kwamba ulipo kuwa duniani ulifanya nini (Luka 9:23).
Wanadamu wana maneno mengi sana ya kuweza kukukatisha tamaa usiweze kufika mahali ambapo Mungu amepakusudia, huo ugonjwa siyo wako, iyo shida siyo yako, na ndiyo maaana Yesu akaja hapa duniani ili mimi na wewe tupate kuokolewa, tusiichezee hii neema kwa sababu utafika wakati ambapo utautafuta wakati kama huu japo usikie maneno ya Mungu, lakini utakuwa umechelewa na hivyo watumishi wa Mungu watakuwa wametwaliwa, hutapata wakati na fursa nyingine ya kutubu Zaidi ya kujikomboa kwa damu yako mwenyewe. Yesu alijitoa akafa pale msalabani, damu yake iliyomwagika pale msalabani ni ya thamani na ni hiyo tu ambayo inaleta ondoleo la dhambi, na hii damu ikipita katika maisha yako, inakomesha magonjwa yote (hata ambayo yameshindikana au yasiyo na taba), maumivu na uchungu vyote vinaisha. Haijalishi umeugua kwa kipindi gani, ikafika sehemu watu wakakupa majina ya “mzee wa ugonjwa”, yupo Yesu, mbona aliponya wengi tu? Hata wewe anakwenda kukuponya ukibadili historia yako (yaani ukiayaacha ya kale na kumkiri yeye kuwa ndiye BWANA na mwokozi wa maisha yako). Kubali kubadili istoria yako ili kubadili msitakabali wa maisha yako ndugu yangu.
Wapo watu wengine wamatamani sana kutoka na kuacha mambo yote mabaya ambayo yanaharaibu historia yao, na wanayo nia ya dhati lakini wanashindwa, na wakati mwingine wamelisikia neno la Mungu na wakaamua kuwa wnakwenda kuokoka, wanatoka kwao wanakwenda makanisani au kwenye mikutano lakini wakifika wanajikuta wanakosa ujasiri au wanajitia moyo kwa kusema nitokoka kesho; ziko nguvu zimewakamata watu kwa sababu ya maagano ambayo yanawafunga watu. Ukizingatia katika maagano tunataegemea kutakuwa na makubaliano au viapo ambavyo vinaweza kuambatana na sadaka yapo maagano ya aina nyingi;
i) Agano la Kimungu
ii) Agano la kishetani
Mungu akubariki sana,na akutunze, fuatilia sehemu ya tano ya somo hili hapo kesho.
By, Ev.Dr Ayubu Mathias Kwandikwa.
LOVE OF CHRIST TO ALL NATIONS(LoCN) is a Ministry that is Committed to Preach the Word of God, as this is what Jesus Ordered to his Disciples. This is Fundamentals for all Christians, and this is his wishes, that everyone hears his word, as preachers and Missionaries we're really committed to achieve this Goal, and if you wish to join us let you be blessed and pray for us.
YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!
- A SALVATION TO ALL NATIONS (ASANA)
- We're delightly to preach the word of almighty God
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment