YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!

My photo
We're delightly to preach the word of almighty God

Thursday, April 27, 2017

SEHEMU YA TATU YA SOMO LENYE KICHWA KIITWACHO "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA

SEHEMU YA TATU YA SOMO LENYE KICHWA KIITWACHO "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA"
     
    AINA ZA HISTORIA
Zipo aina nyingi za historia kulingana na mtazamo wa mwandishi na kile alicho kilenga kuweza kukieleza kwa jamii, kama ambavyo sheria inaweza ikatazama kosa moja kwa macho mawili, mfano mtu anapo ua, wanasheria wanaweza wakalichukulia tukio hilo katika sura mbili;
a) Kuwa mtu huyu pengine aliua bila kukusudia. Ni kweli kabisa kuwa kaua, lakini hakudhamiria (kukusudia) kufanya hivyo, mfano askari wakiwa doria, hakuna aliyepanga kuwa anakwenda huko (kwenye doria) ili kuua, lakini inatokea uvamizi na wavamizi wanapewa ishara ya kujisalimisha lakini wanakaidi kauli hiyo na kuanza kuwarushia risasi askari. Askari wataanza kujibu kwa risasi, ikitokea jambazi kaua, hatuwezi kusema askari alidhamilia (kusudia) kuua.
b) Kuwa kaua kwa kukusudia. Kwamba ni kweli amejiandaa kwaajili ya kuua. Mfano tulimuona mtuhumiwa akinunua upanga na kuunoa tangu juzi na aliwahi kumtamukia marehemu kuwa nitakuua kwa upanga, na leo kweli kafanya vile.
 Lakini kwangu mimi naichukulia historia katika mtazamo wa aina mbili, na aina hizi mbili ni;
Historia ya maisha ya mtu kabla hajamfahamu Yesu, yaani kabla mtu hajampokea Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yake.
Historia ya maisha ya mtu baada ya kumpokea Yesu Kristo, yaani mtu akiisha kukubali kumpokea Yesu kristo kuwa ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yake.( ukiwa ndani ya kristo tazama umekuwa kiumbe kipya na mambo ya kale yamepita) & Danieli 5:25- MENE, MENE TEKELI, NA PERESI,
Mungu akutunze, fuatilia sehemu ya nne ya somo hili kesho.
By Ev.Dr Ayubu Mathias Kwandikwa.

No comments:

Post a Comment