YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!

My photo
We're delightly to preach the word of almighty God

Tuesday, April 25, 2017

TUNAKULETEA MFULULIZO WA SOMO LINALOITWA "NAMNA YA KUJITOA KATIKA HISTORIA YAKO"

Namna ya kujitoa katika kifungo cha Historia yako”, ni ujumbe ambao Mungu alinipa baada kupata shida katika utumishi wangu. Maana Historia yangu ilikuwa ni mzigo mkubwa kwangu hasa nilipoamua kumtumikia Mungu katika Roho na kweli. Wapo watu nilipo waambia kwa habari ya uamuzi wangu, walinicheka sana na kunambia tumekuzoea, wewe ni wa hivyohivyo. Kimsingi nilikata tama asana katika utumishi wangu kwa maneno ya watu wale, maana wanachokisema ni kweli kabisa katika mtazamo wa kibinadamu haiwezekani kuacha. Ikafika sehemu nikasema nisimtumikie Mungu, nikawa naishi bila matumaini, nikawa sina Amani kabisa tena katika maisha yangu.
     Lakini namshukuru Mungu ambaye aliamua kuniinulia watua ambao walisimama na kunitia moyo. Siku moja nikawa nasoma Habari ya Paulo (Sauli) ambavyo alikuwa akiwaua watumishi wa Mungu lakini Mungu alivyoamua kuwa Paulo amtumikie, Paulo alimtumikia Mungu japo kwa mazingira magumu, watu wasingeweza kumuamini Paulo kuwa kweli ni mtumishi wa Mungu kw asiku hizi. Lakini Paulo pia hakuweza kuwaangalia wanadamu wanasema nini, alimwanngalia yeye aliyempa kazi ile. Tangu baada ya kusoma ujumbe huo ndipo nilipo pata nguvu ya kuendelea, nikasema lazima nitumike haijarishi historia yangu ilikuwaje.
  Nina wiwa kukuletea ujumbe huu, uupokee kwa shauku kubwa na kutegemea kupata kitu katika maisha yako na Mungu atakwenda kukugusa na kukusaidia. Haijalishi ulikuwa na historia ya namna gani, yuko Yesu ambaye ataifuta historia hiyo na kukupa nguvu za kuendelea mbele. Kitu cha msingi ni “Ukubali kufanya vile anavyokuagiza”.

















No comments:

Post a Comment