Agano la Kimungu, hili ni lile agano ambalo mtu anafanya na Mungu katika madhabahu yake, mtu anakuwa anahitaji msaada kutoka kwa Mungu hivyo anafanya makubaliano yake na Mungu ili Mungu aingilie kati katika shida yake, au mtu anafanya agano na Mungu kwa sababu tu kamuona Mungu akifanya vitu katika maisha yake; mfano mzuri ni Yoshua pale alipowaambia wana waisraeli kuwa “Chagueni hivi leo mtakaye mtumikia; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA” , Yoshua aliapa yeye kama yeye lakini pia katika kuapa kwake akaiapia na familia yake (mke na watoto wake).
Agano la kishetani, hili nia agano baina ya mtu na miungu, mapepo, majini,na mizimu. Na agano hili linaambatana na kutoa sadaka ya uhai wa mtu au wanyama wengine. Viapo vilivyopo hapa
Kumekuwa na shida kubwa sana kwa watu kubadili historia za maisha yao, vipo vifungo mbalimbali ambavyo mtu kabla hajampokea Yesu kristo anakuwa kafungwa kwenye hivyo vifungo. Hasa mtu kama alikuwa na tabia mbaya ambazo karibia kila mtu akawa anafahamu kuwa yeye ni mtu mwenye tabia hiyo na hasa watu wakaanza kutazama uwezekano wa kuweza mtu huyo kubadilika.
LOVE OF CHRIST TO ALL NATIONS(LoCN)
LOVE OF CHRIST TO ALL NATIONS(LoCN) is a Ministry that is Committed to Preach the Word of God, as this is what Jesus Ordered to his Disciples. This is Fundamentals for all Christians, and this is his wishes, that everyone hears his word, as preachers and Missionaries we're really committed to achieve this Goal, and if you wish to join us let you be blessed and pray for us.
YESU ANAWEZA KUKUTOA KATIKA SHIDA ULIYONAYO, AMINI TU!
- A SALVATION TO ALL NATIONS (ASANA)
- We're delightly to preach the word of almighty God
Saturday, June 16, 2018
ARE YOU UPSETTED UP BY LIFE?
Praise the Lord!? We are glady to meet you again, for a while we have not been in the position to share with you the words of God for the reasons that were above our capability. But we are back now.
Sometimes the hard time we are walking through we become so discouraged. But I want to remind you that God I keeping a look, so speak to yourself that your the most successful person in this world.
One of the big mistake a man can do, is not to trust himself because is not trusted by others.
You were born alone, there were millions of sperms that were to fertilize a single egg, a sperm that encouraged itself it worn the game and that's you.
Your running with a lot of plans, with our friends, our works and many others, but don't loose your focus.
By Ayubu Mathias (Executive Manager Amakwani Medical Center - AMC Katoro Geita).

Sunday, April 30, 2017
SEHEMU YA SITA YA SOMO LENYE KICHWA "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA". HISTORIA YA MTU NA HATIMA YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKE:
Historia ya mtu inamchango mkubwa sana katika mafanikio katika maisha yake ya kimwili na kiroho, jinsi ambavyo utatengeneza mazingira ya kupata kitu Fulani kuna uwezekano mkubwa wa kukipata ukilinganisha na vile ambavyo hukuandaa mazingira ya kitu hicho.
Hivyo historia ya mtu inakuwa na nafasi kubwa katika maisha ya mtu kwa sababu;
Inaweza kutoa hatima ya mafanikio ya mtu katika maisha yake.
Inaweza kumjengea msingi mzuri au mbaya katika maisha yake.
Inaweza kuamua hatima ya watu atakao kuwa nao katika maisha kama vile marafiki, ndugu jamaa na watu wengine.
Zipo historia za namana mbili ambazo wewe kama mtumishi wa Mungu lazima uzifahamu;
Danieli alikuwa na historia njema katika maisha yake, Danieli 6:1-24
Mfano mzuri ni Mtume Paulo( aliyekuwa Sauli hapo awali)- MATENDO 8:1-
Mungu akubariki, fuatilia sehemu ya saba ya somo letu hapo kesho.
By Ev. Dr Ayubu Mathias Kwandikwa.
Saturday, April 29, 2017
SEHEMU YA TANO YA SOMO LENYE KICHWA "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA"
Jana tuliishia pale tulipo orodhesha aina mbili za maagano, sasa tuyatazame kwa ufupi
1.Agano la Kimungu, hili ni lile agano ambalo mtu anafanya na Mungu katika madhabahu yake, mtu anakuwa anahitaji msaada kutoka kwa Mungu hivyo anafanya makubaliano yake na Mungu ili Mungu aingilie kati katika shida yake, au mtu anafanya agano na Mungu kwa sababu tu kamuona Mungu akifanya vitu katika maisha yake; mfano mzuri ni Yoshua pale alipowaambia wana waisraeli kuwa “Chagueni hivi leo mtakaye mtumikia; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA” , Yoshua aliapa yeye kama yeye lakini pia katika kuapa kwake akaiapia na familia yake (mke na watoto wake).
2. Agano la kishetani, hili nia agano baina ya mtu na miungu, mapepo, majini,na mizimu. Na agano hili linaambatana na kutoa sadaka ya uhai wa mtu au wanyama wengine. Viapo vilivyopo hapa
Kumekuwa na shida kubwa sana kwa watu kubadili historia za maisha yao, vipo vifungo mbalimbali ambavyo mtu kabla hajampokea Yesu kristo anakuwa kafungwa kwenye hivyo vifungo. Hasa mtu kama alikuwa na tabia mbaya ambazo karibia kila mtu akawa anafahamu kuwa yeye ni mtu mwenye tabia hiyo na hasa watu wakaanza kutazama uwezekano wa kuweza mtu huyo kubadilika.
Mungu akutunze, fuatilia sehemu ya sita hapo kesho.
By Ev. Ayubu Mathias Kwandikwa.

Friday, April 28, 2017
SEHEMU YA NNE YA SOMO LENYE KICHWA "NAMNA YA KUJITOA KATIKA KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA"
AINA YA KWANZA
I. HISTORIA YA MTU KABLA YA KUMFAHAMU YESU KRISTO NA KUMPOKEA KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE:
Hii inakuwa ni ile historia anayokuwa nayo kila mtu. Hii ni lazima utaipitia tu, na ni kwa sababu hakuna aliyezaliwa akiwa amemuamini Yesu Kristo kuwa ni BWANA na mwokozi wa maisha yake. Na hapa bado watu wengi hawajafahamu kuwa ukizaliwa katika familia ya kikristo haina maana kwamba tayari umempokea Yesu Kristo na kumkubali kuwa ndiye mwokozi wa maisha yako. Kumpokea ni sehemu ya kwanza lakini pia kumkubali kuwa ndiye BWANA na mwokozi wa maisha yako ni sehemu ya pili. Na Biblia imeweka bayana kabisa kwa habari ya kumfuata na kumkubali Yesu (Luka 12:8-9), haina sababu ya kuendelea kuwa unadhani uko upande Fulani lakini kumbe hauko upande huo,sasa ni muhimu sana kuwa makini kwa hili. Kumfuata Yesu ni lazima ujikane mwenyewe, siyo suala la kukuta wazazi wako wana Sali, na wewe ukaamini kuwa tayari haina haja ya kuokoka (yaani kumkiri Yesu kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako, yaani uokoke kwa kumkiri kwa maneno ya kinywa chako). Kati ya vitu ambavyo vimenisumbua katika maisha yangu ni kuhusu kuokoka huku tayari nilikuwa ni kisimama majukwaani kwenye mikutano na kuhubiri, nimesimama kwenye madhabahu na kuhudumu, lakini bado nikawa sina Amani.
Roho yangu ilikosa Amani kwa sababu nimezaliwa katika familia ya kikristo na kukulia katika familia ya kikristo, lakini bado nilidhani kuwa haina haja ya kuokoka maana ukizaliwa katika familia ya kikristo tayari utakuwa umeokoka, lakini sikweli, ni lazima umkiri Yesu kwa kinywa chako mwenyewe (Warumi 10:9-11), hivyo huwezi okolewa wala kuwa katika ufalme wa Mungu kama hujamkiri kwa kinywa chako wewe mwenyewe. Mungu akujalie kuelewa ujumbe huu, jitahidi uelewe kitu gani Mungu anakihitaji kwako wewe mwanadamu aliyekufilia pale msalabani.
Ikawa siku moja Roho wa BWANA akawa ananisihi niokoke, lakini maswali makubwa yaliyokuwa kichwani mwangu ni; hivi kweli sijaokoka? Hivi watu watanichukuliaje? Si nitazua maada vichwani kwa watu kwamba alikuwa anasimama kuhubiri, leo imekuwaje? Au katenda dhambi jana?Lakini kile nilichokifanya ni kulitazama neno la Mungu linasemaje, nakumbuka ilikuwa ni kwenye semina katika kanisa moja lililoko mkoani Ruvuma, ndipo aliposimama mama mmoja kufundisha katika ile semina, na ndipo somo alilotufundisha likawa na majibu ya kile kilichonisumbua siku nyingi, ndipo nilipoamua mwenyewe kuokoka.
Baada nikawa na amani moyoni mwangu. Yesu anawambia wanafunzi wake kuwa anayetaka kunifuata lazima ajikane yeye mwenyewe (Luka 9:23), maana yake uamue wewe mwenyewe bila kufanya hivyo kwa sababu pengine umezaliwa ukakuta ni kama desturi kwenda kanisani na leo unatembea na kusema umeokoka, lakini kumbuka Yesu mwenyewe anasema kila mtu atakaye mkiri mbele ya watu, hata yeye atamkiri mbele ya Baba yake aliye mbinguni (Mathayo 10:32). Na bahati mbaya wengine tayari ni viongozi, ni watu wa kubwa wana majina yenye sifa na hivyo wanaogopa kukiri na kujishusha, (Yohana 12:42). Usiogope eti watu watakutenga, ni bora wakutenge lakini uurithi ufalme wa Mungu, kwani utapata faida gani endapo wanadamu watakuona umeokoka lakini kumbe Mungu hakutambui?.Ule wakati wa kukata kauri unafika ambapo hatima ya kila mtu itajulikana kuwa ulikuwa wa Mungu au laa! Ionekane kuwa kumbe mhubiri ulikuwa hujaokoka?, mchungaji ulikuwa hujaokoka? Muimbaji ulikuwa hujaokoka? Inauma sana, maana unautumia muda wako kumtumikia Mungu lakini hakutambui.
Historia tunayo zaliwa nayo kwa kawaida ndiyo inayoendelea kutujengea kesho yetu sisi, sasa usipokuwa makini itakuwa ni shida sana. Ni kweli yamkini hukuzaliwa katika familia ya kikristo , lakini umeishi maisha ambayo hayampendezi Mungu, bado ipo nafasi ya kuweza kurekebisha nafasi hiyo na kuibadilisha historia yako, watu walizoea kukuona wewe ni mzinzi lakini leo acha huo uzinzi, watu walizoea kukuona ukitukana, ukilewa pombe,ukitoa matusi, ukifanya udharirishaji, ukiiba, ukisaliti, ukifanya mambo yasiyo mpendeza Mungu, achana yano, njoo kwa Yesu.Yesu anakupenda sana ndiyo maana umepata nafasi nyiningine hii hata yakuweza kusoma ujumbe huu.
Mfano mzuri ni Mtume Paulo (aliyekuwa Sauli hapo awali) Matendo 8:1- . Alikuwa mtu ambaye anaogopeka sana kwa sababu alikuwa akiwaua watumishi wa Mungu, katika kipindi hiki, ni kipindi ambacho kinakumbukwa sana kwa maana ni kipindi ambacho kanisa lilipata wakati mgumu, Amani ilitoweka, waumini wa kanisa pia walipata wakati mgumu. Lakini kwao mitume ilikuwa ni tofauti kabisa maana kabla ya kipindi hiki Yesu alijua wakati huu mgumu ambao kanisa linakwenda kuupitia na ndiyo maana alisisitiza mitume wajazwe na Roho mtakatifu, maana bila ya Roho mtakatifu wasingeweza kustahimiri mateso ambayo yaliwakabili katika kipindi hicho. Sauli alitumika kutimiza kusudi la kipindi kile, aliwaua mitume wengi sana, ikafika kipindi akawa anaogopeka sana hata anapoonekana mtaani hata kama hana mpango wa kufanya mauaji, kwake alikuwa akijisikia viziri sana kufanya vile, wakuu wa sharia walimtumia sana maana hakuwahi kushindwa kufanya kitu ambacho walikuwa wakimuagiza afanye. Hivyo alijikuta anaogopeka sana,na historia yake ikajengeka kuwa huyu mtu siyo wa kawaida hata kidogo, kwa hali ya kawaida Sauli alikuwa siyo mtu wa kawaida maana tabia na mwenendo wake vilikuwa vinatisha, na hata mitume walipomuona Sauli walikuwa wanatambua kuwa yamkini leo ni mwisho wao. Historia yake ikajengwa katika misingi ya kuogofya, akawa ni mtu anyeogopeka kila mahali kwa sababu ya matendo yake hayo.
Lakini nataka nikwambie kitu kimoja ndugu yangu, ni bora wanadamu wakuone hufai na hunathaamani lakini ukampata Yesu, yeye ni wathamani. Haohao ambao wanakushangaa na kukuona hufai na wakikuona ukifanya vile wanavyotaka ndiyo wanafurahi, kumbuka wao pia ni wanadamu, ipo siku watakufa (Ayubu 14:1-2). Yesu yeye yupo milele yote, anasema yeye ni yule yule jana na leo na hata milele, ukiwa na Yesu hatakuacha katika shida yako, yeye hatakufa, kwahiyo ukimtegemea yeye inakuwa ni bora sana kwa sababu yeye hafi yupo milele yote.
Wengine wanaogopa kuokoka kwa sababu wanajua wameishi maisha yasiyompendeza Mungu hata wanadamu, hivyo wanaona kwamba hivi wanadamu wataamini kuwa kweli tumeokoka na kuacha dhambi zetu? Nataka nikwambie kuwa hauokoki ili kumfanya jirani yako, mzazi wako, rafiki yako au mwanadamu yeyote ajue kuwa umeokoka! Bali unaamua kuokoka ili kuyaponya maisha yako, haina maana ya kuwasikiliza wanadamu huku wanadamu hawana mbingu yeyote ya kukupeleka. Usiogope wanadamu wanasema nini, bali tazama kuwa maisha ya hapa duniani yanapita, iko sehemu Mungu ameiandaa kwaajili yako. Usiwaogope wanadamu kwa sababu ukiwaogopa wanadamu ukakataa kumkiri Yesu ile mbingu siyo kwaajili yako (Luka 9:26), usiwaangalie marafiki, ndugu zako au wazazi wako wanasema nini kwa sababu siku ile ya mwisho utasimama wewe kama wewe ili utoe hesabu yako, kwamba ulipo kuwa duniani ulifanya nini (Luka 9:23).
Wanadamu wana maneno mengi sana ya kuweza kukukatisha tamaa usiweze kufika mahali ambapo Mungu amepakusudia, huo ugonjwa siyo wako, iyo shida siyo yako, na ndiyo maaana Yesu akaja hapa duniani ili mimi na wewe tupate kuokolewa, tusiichezee hii neema kwa sababu utafika wakati ambapo utautafuta wakati kama huu japo usikie maneno ya Mungu, lakini utakuwa umechelewa na hivyo watumishi wa Mungu watakuwa wametwaliwa, hutapata wakati na fursa nyingine ya kutubu Zaidi ya kujikomboa kwa damu yako mwenyewe. Yesu alijitoa akafa pale msalabani, damu yake iliyomwagika pale msalabani ni ya thamani na ni hiyo tu ambayo inaleta ondoleo la dhambi, na hii damu ikipita katika maisha yako, inakomesha magonjwa yote (hata ambayo yameshindikana au yasiyo na taba), maumivu na uchungu vyote vinaisha. Haijalishi umeugua kwa kipindi gani, ikafika sehemu watu wakakupa majina ya “mzee wa ugonjwa”, yupo Yesu, mbona aliponya wengi tu? Hata wewe anakwenda kukuponya ukibadili historia yako (yaani ukiayaacha ya kale na kumkiri yeye kuwa ndiye BWANA na mwokozi wa maisha yako). Kubali kubadili istoria yako ili kubadili msitakabali wa maisha yako ndugu yangu.
Wapo watu wengine wamatamani sana kutoka na kuacha mambo yote mabaya ambayo yanaharaibu historia yao, na wanayo nia ya dhati lakini wanashindwa, na wakati mwingine wamelisikia neno la Mungu na wakaamua kuwa wnakwenda kuokoka, wanatoka kwao wanakwenda makanisani au kwenye mikutano lakini wakifika wanajikuta wanakosa ujasiri au wanajitia moyo kwa kusema nitokoka kesho; ziko nguvu zimewakamata watu kwa sababu ya maagano ambayo yanawafunga watu. Ukizingatia katika maagano tunataegemea kutakuwa na makubaliano au viapo ambavyo vinaweza kuambatana na sadaka yapo maagano ya aina nyingi;
i) Agano la Kimungu
ii) Agano la kishetani
Mungu akubariki sana,na akutunze, fuatilia sehemu ya tano ya somo hili hapo kesho.
By, Ev.Dr Ayubu Mathias Kwandikwa.

Thursday, April 27, 2017
SEHEMU YA TATU YA SOMO LENYE KICHWA KIITWACHO "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA
SEHEMU YA TATU YA SOMO LENYE KICHWA KIITWACHO "NAMNA YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA HISTORIA YAKO YA NYUMA"
AINA ZA HISTORIA
Zipo aina nyingi za historia kulingana na mtazamo wa mwandishi na kile alicho kilenga kuweza kukieleza kwa jamii, kama ambavyo sheria inaweza ikatazama kosa moja kwa macho mawili, mfano mtu anapo ua, wanasheria wanaweza wakalichukulia tukio hilo katika sura mbili;
a) Kuwa mtu huyu pengine aliua bila kukusudia. Ni kweli kabisa kuwa kaua, lakini hakudhamiria (kukusudia) kufanya hivyo, mfano askari wakiwa doria, hakuna aliyepanga kuwa anakwenda huko (kwenye doria) ili kuua, lakini inatokea uvamizi na wavamizi wanapewa ishara ya kujisalimisha lakini wanakaidi kauli hiyo na kuanza kuwarushia risasi askari. Askari wataanza kujibu kwa risasi, ikitokea jambazi kaua, hatuwezi kusema askari alidhamilia (kusudia) kuua.
b) Kuwa kaua kwa kukusudia. Kwamba ni kweli amejiandaa kwaajili ya kuua. Mfano tulimuona mtuhumiwa akinunua upanga na kuunoa tangu juzi na aliwahi kumtamukia marehemu kuwa nitakuua kwa upanga, na leo kweli kafanya vile.
Lakini kwangu mimi naichukulia historia katika mtazamo wa aina mbili, na aina hizi mbili ni;
Historia ya maisha ya mtu kabla hajamfahamu Yesu, yaani kabla mtu hajampokea Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yake.
Historia ya maisha ya mtu baada ya kumpokea Yesu Kristo, yaani mtu akiisha kukubali kumpokea Yesu kristo kuwa ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yake.( ukiwa ndani ya kristo tazama umekuwa kiumbe kipya na mambo ya kale yamepita) & Danieli 5:25- MENE, MENE TEKELI, NA PERESI,
Mungu akutunze, fuatilia sehemu ya nne ya somo hili kesho.
By Ev.Dr Ayubu Mathias Kwandikwa.

Wednesday, April 26, 2017
Sehemu ya pili ya somo letu lenye kichwa kiitwacho "NAMNA YA KUJITOA KATIKA HISTORIA YAKO YA NYUMA
MAANA YA HISTORIA
Ninapo zungumza kwa habari ya historia, ninakuwa ninazungumzia jumla ya namna ambavyo mtu ameishi na watu, na kufanya vitu ambavyo vikajenga kumbukumbu katika maisha yake, pamoja kwamba huyo mtu anaweza akasahau au akakumbuka, kumbukumbu hiyo pia yaweza kuwa njema au siyo njema machoni kwa watu au kwa mtu yule (yaani mhusika). Na siku zote vile vitu vizuri vinaweza vikasahaulika kwa haraka zaidi lakini vile vitu vibaya inakuwa ni vigumu kusahaulika kwa sababu vinaumiza mioyo ya watu na kutia doa, na mara nyingi doa hilo likitazamwa na moyo huonekana na kuleta kumbukumbu ya kisababishi cha doa hilo. Mfano mzuri ni pale tunapomuona mtu alikuwa ni kiongozi mzuri tu, lakini baadaye akafanya jambo baya, huwa anakuja kuonekana kuwa ni mtu mbaya na kosa hilo hufunika mazuri yote ambayo amewahi kuyafanya.
Vitu vyote na shughuli zote ambazo mtu amezipitia kabla ya kufika hapo alipo, tunapo muona leo. Tunaona kwenye misiba mbali mabali, historia ya marehemu inasomwa, wataeleza mambo mengi aliyoyafanya, kama alisoma wataeleza alisoma wapi, watasema sababu ya kifo chake, watasema kaacha watoto wangapi (kama alikuwa na familia) na mengineyo mengi kulingana na utaratibu utakao wekwa. Yako mambo mengi mtu anayokuwa ameyafanya ambayo wakati wa uhai wake hatuwezi kuyafahamu lakini baada ya kifo chake vitu huwa vinakuwa wazi kabisa.
Na historia hubadilika, kwa kuwa tabia ni jumla ya mwenendo wa maisha ya mtu, na tabia ndiyo inayojenga historia ya mtu. Unapozungumza kuhusu historia bila kuzungumzia tabia, ni sawa na kungoja meli uwanja wa ndege. Maana yake ni kwamba, tabia ni kama matofari wakati wa kujenga nyumba, historia ni jumla ya tabia zote ambazo mtu anakuwa amezionyesha kwa kipindi Fulani. Huwezi kusema huyu mtu ana historia mbaya kama umemuona mara moja tu akifanya kitu Fulani kibaya (japo pia inawezekana, kwa sababu jambo hilo linaingia katika historia ya maisha yake), lakini tukizungumza kwa hali ya kawaida, historia ya mtu inabidi ipimwe kwa muda fulani, na ndiyo maana historia inajengwa na tabia mbali mbali, nzuri au mbaya,zote kwa pamoja zinajenga historia ya mtu.
Viko vitu ambavyo vinaweza kuchangia kubadilika kwa tabia na mwenendo (historia) wa mtu;
i) Kitu cha kwanza ni “Msukumo wa ndani ambao kila mtu kazaliwa nao”. Huu ni msukumo ambao ni wa ndani ambao ni wa asili ambao ukija ni lazima uutimize, mfano; Mtu anapata msukumo wa kula (njaa), hapa suluhisho ni moja tu, ambalo ni kula, na siyo kwamba wewe ndo unauleta msukumo huo. Lakini lazima uwe na uwezo wa kuweza kuuthibiti msukumo huo pamoja kwamba ni lazima uutimize.
ii) “Nguvu ya akili”. Akili ni uelewa ambao anakuwa nao mtu, ambao unamsaidia aweze kujitambua, ambao pia unamsaidia akumbuke na ni chanzo cha mawazo ya mtu. Hapa mtu anatumia uelewa wake kwa kujipima kama anastahiri kufanya kitu Fulani, na kama anatakiwa afanye kitu Fulani, je! Afanye kwa wakati upi?, pia mtu hapa anaangalia madhara yay eye kuweza kufanya kitu Fulani, ni kweli kwamba huu ni msukumo wa ndani ambao kwa hali ya kawaida ni lazima ni fanye, lakini je! Ni lazima nifanye? Na kama ni lazima nifanye,je! Ni lazima nifanye kwa wakati huu? Nikifanya jamii itanitazama vipi? Je! thamani yangu itashuka kwa jamii ninayoishi? Kama inatakiwa nifanye,je! Nilazima nifanye kwa mtindo huu?. Hapa mtu anjitathmini kufanya kitu Fulani ambacho kinasababishwa na msukumo wa ndani, lakini yeye anajaribu kutazama thamani yake katika jamii, kwamba je! Kile kitu kinakubalika katika jamii anayoiishi?. Jambo hili la pili ninaweza nikasema ni la mhimu sana kwa sababu linakitazama kitu kabla hujakifanya, linakitathmini kulingana na sheria na taratibu ambavyo zinavyohitaji na kutoa tafsiri ya kile kitu, ili mtu aepukane na aibu na kuvunjika kwa heshima yake katika jamii.
iii) Nguvu kuu, hii ni nguvu ambayo ndani yake imebeba akili, ambayo kwa kawaida inajitegemea, na kuweka bayana uelewa na uhalisi wa mambo. Hii ni nguvu ambayo inuwezo wa kuthibiti “nguvu ya msukumo wa ndani” na nguvu ya akili. Hii inakagua na kutazama vile vitu ambavyo mtu kavifanya, je! Ni sahihi kufanywa, na kama ni sahihi, je! Ni kwa namna ilivyotakiwa kufanywa? Na je! Ni kwa wakati ambao vilitakiwa kufanywa?. Hii nguvu inawakilisha jukumu la wazazi, sharia na taratibu za nchi, sharia na taratibu za kidini. Lakini kwetu sisi, hii nguvu ni ile sharia na taratibu ambazo Mungu kaziweka kwetu sisi. Na kushindwa kuzingatia sharia hii ni sawa na kuandaa bomu ambalo litakulipua wewe mwenyewe. Vitu vyote vile viwili vya mwanzo vinaweza vikashindwa lakini kitu hiki cha mwisho ni cha muhimu na cha msingi sana katika maisha yako wewe kama mkristo. Rumi 7:23-25
Historia inajengwa na vitu vyote hivyo vitatu vilivyotajwa hapo juu, na historia yako kuwa mbaya au nzuri inategemea sana jinsi ambavyo hivyo vitu vitatu umevitazama vipi na umeviweka vipi katika maisha yako, ni kweli kabisa kuwa ni vigumu kuweza kuepuka vitu vingine, lakini inawezekana maana palipo na nia pana njia; Wafilipi 4:13. Historia yako itakuwa njema nay a kuigwa kama hutatumia akili zako wewe mwenyewe, maana peke yako hutaweza. Wako watu wao huwa wanasema huwezi kuwa mtakatifu ukiwa duniani, mimi ninapingana nao vikali kabisa; Zaburi 16:3, hana maana kwamba watakatifu walioko mbinguni hawathamini, ni kwa sababu tu kuwa hawa watakatifu walioko duniani wamekuwa ni watakatifu, licha ya kuwa wanaishi katika ulimwengu wa dhambi lakini wamekuwa ni watakatifu.
Ukisoma habari ya mfalme Hezekia, Isaya 38:1-8, anatokewa na nabii Isaya mwana wa Amozi kwa habari ya ugonjwa wake, anaambiwa Hezekia hutapona bali utakufa; Hezekia “akasema, Ee BWANA, kumbuka haya”, huwezi kumwambia mtu akumbuke kama hukumaanisha kuwa aangalie vitu au kitu ambacho ni muhimu ambacho umewahi kukifanya katika maisha yako ambacho kikitazamwa kinaleta maana kubwa wakati huo. Yako mambo aliyoyafanya mfalme Hezekia, yakajenga historia ya maisha yake ambayo Mungu akiyatazama anaona kweli huyu mtu kakamilika. Yako mambo makubwa aliyafanya Hezekia na Biblia inamsifu inasema hakuna mfalme aliyekuwa mzuri kabla na baada yake , 2Nyakati 18:1-8.
Jinsi ambavyo unaweza ukaishi leo ndivyo ambavyo unakuwa unaiandaa kesho yako. Vile alivyoishi mfalme Hezekia ndivyo alivyompendeza Mungu, ndiyo maana tunamuona mfalme Hezekia anpata neema kuu tatu machoni mwa Mungu;
i) Kujua wakati wake wa kufa. Kupewa taarifa kuwa atakufa wakati huu.
ii) Kushauriwa kitu cha kufanya, maana aliambiwa hatapona bali atakufa, hivyo atengeneze mambo ya nyumba yake. Na ushauri mzuri ni ule atakao kupa Mungu, maana anakuwa na uhakika nao, lakini unakuwa ni uhakika wa kweli.
iii) Kuongezewa miaka ya uhai wake. Baada ya mfalme Hezekia kupewa taarifa kuwa atakufa wala hatadumu, alichokifanya hakung’ang’ana na nabii Isaya, bali aligeuza uso wake kwenye ukuta na kumwita Mungu na akamwambia akumbuke jinsi alivyoenenda kwa ukamilifu mbele zake.
Hii ni heshima kubwa kati ya heshima ambazo Mungu amewahi kuzionyesha kwa mwanadamu, Hezekia alipata heshima kubwa na upendeleo mkubwa sana, yaani kule kupewa taarifa tu kuwa aandae mambo ya nyumba yake maana atakufa wala hatapona; ni neema kubwa mno, ni watu wangapi wamewahi kupata neema hiyo?Kwa watu wa leo wangesema ya kuwa basi kwa kuwa amesema nitakufa ngoja nimalizie raha na niombe msamaha ili nife katika maisha matakatifu. Wapo watu wanakufa na baadae ndugu zao wanakwenda kuwaombea makanisani ili wapate rehema, wanasahau neno la Mungu linasemaje katika neno lake; Waebrania 9:27. Kila mtu atabeba mzigo wake yeye mwenyewe, atawjibika kwa kile alichokifanya akiwa hapa duniani, historia yako imebeba maana kubwa na kuonyeshs njia unayopaswa kuingia.
Mungu akutunze, tukutane hapo kesho,by Ev.Dr Ayubu Mathias Kwandikwa
Tuesday, April 25, 2017
TUNAKULETEA MFULULIZO WA SOMO LINALOITWA "NAMNA YA KUJITOA KATIKA HISTORIA YAKO"
Namna ya kujitoa katika kifungo cha Historia yako”, ni ujumbe ambao Mungu alinipa baada kupata shida katika utumishi wangu. Maana Historia yangu ilikuwa ni mzigo mkubwa kwangu hasa nilipoamua kumtumikia Mungu katika Roho na kweli. Wapo watu nilipo waambia kwa habari ya uamuzi wangu, walinicheka sana na kunambia tumekuzoea, wewe ni wa hivyohivyo. Kimsingi nilikata tama asana katika utumishi wangu kwa maneno ya watu wale, maana wanachokisema ni kweli kabisa katika mtazamo wa kibinadamu haiwezekani kuacha. Ikafika sehemu nikasema nisimtumikie Mungu, nikawa naishi bila matumaini, nikawa sina Amani kabisa tena katika maisha yangu.
Lakini namshukuru Mungu ambaye aliamua kuniinulia watua ambao walisimama na kunitia moyo. Siku moja nikawa nasoma Habari ya Paulo (Sauli) ambavyo alikuwa akiwaua watumishi wa Mungu lakini Mungu alivyoamua kuwa Paulo amtumikie, Paulo alimtumikia Mungu japo kwa mazingira magumu, watu wasingeweza kumuamini Paulo kuwa kweli ni mtumishi wa Mungu kw asiku hizi. Lakini Paulo pia hakuweza kuwaangalia wanadamu wanasema nini, alimwanngalia yeye aliyempa kazi ile. Tangu baada ya kusoma ujumbe huo ndipo nilipo pata nguvu ya kuendelea, nikasema lazima nitumike haijarishi historia yangu ilikuwaje.
Nina wiwa kukuletea ujumbe huu, uupokee kwa shauku kubwa na kutegemea kupata kitu katika maisha yako na Mungu atakwenda kukugusa na kukusaidia. Haijalishi ulikuwa na historia ya namna gani, yuko Yesu ambaye ataifuta historia hiyo na kukupa nguvu za kuendelea mbele. Kitu cha msingi ni “Ukubali kufanya vile anavyokuagiza”.

Monday, April 24, 2017
SOMO: WEKA ALAMA YA UKOMBOZI KATIKA MAISHA YAKO
Alama ni nini? Ni kielekezo au ishara ambayo inawekwa au inakuwepo kuweza kutambulisha kitu Fulani. Tumekuwa tukiona sehemu mbalimbali kwa wafanyakazi wa mahali fulania au wanafunzi wanakuwa wanapewa vitambulisho, hivi ni alama ambazo zinawafanya watambuliwe.
KUTOKA 12:7-13, 21
Utakumbuka wana waisraeli walipokuwa utumwani huko Misri, walipata shida kubwa sana, wakamlilia Mungu wao. Haikuwa rahisi kwao wana waisraeli kuweza kupewa kibali, na walipopewa kibali bado adui yao hakuchoka kuwafuatilia. Hivyo sisi kama wakristo tusifike sehemu tukaona Mungu ametusaidia halafu tukaamua kumsahau, tuwe na uhakika Zaidi kuwa kila baada ya kupata ushindi katika jaribu Fulani( vita ) , adui zetu huwa wanajipanga Zaidi ili kuja kutuangusha, ndivyo ilivyokuwa kwa wana waisraeli, Farao aliyekuwa mfame wa ‘[Misri alipokataa kuwapatia ruhusa wana waisreli, Mungu aliamua kuachilia mapigo kumi (10) ,pigo la mwisho ni lile la kufa kwa wazaliwa wote wa kwanza wa Misri huku wana waisreli wakiwa salama kabisa. Unaona damu ya mwana kondoo ambavyo inatumiwa kama alama ya kuweza kutuepushia kila aina ya taabu kubwa au kuwa kinga kubwa katika maisha yetu.
Unajua kama wasingeweka damu katika milango yao, pia wao wangeweza kupatwa na vifo sawa na vile vilivyowapata wamisri? Unajua mtu wa Mungu, Mungu anavyokwambia fanya hivi, jitahidi kufanya hivyo, maana kwa kufanya hivyo unakuwa unajiwekea alama ambayo itamfanya Mungu wakati akiwa anapita kubariki watu wake asije akakusahau au wakati akiwa anaangamiza asikuangamize. Na wana waisraeli waliambiwa wakae ndani ya nyumba zao, wala wasijetoka nje ambapo wakati wa usiku wa manane Malaika wa uangamivu atakapokuwa akipita asiweze kuwaangamiza.
Baada ya Farao kuwapa ruhusa kwamba waondoke, bado aliwafuatilia tena kuhakikisha kuwa hawaondoki. Ndivyo unapoona umewashinda adui zako, usiwe ni wakati wa kubweteka na kuridhika, huo ndiyo wakati mzuri wa kumtafuta Mungu ili aonekane Zaidi katika maisha yako. Watu wengi wamekuwa wakikutana na shida wanamkumbuka Mungu, lakini baada ya shida zao kuisha wanamsahau Mungu, wanashindwa kujua tayari wametangaza vita na adui, halafu wanakimbilia maeneo yasiyokuwa salama(yasiyokuwa na ulinzi).
Wana waisraeli walipata taabu njiani lakini kubwa kuliko huwa ni pale walipofika mwisho wa njia yao( walipofika katika bahari ya shamu). Lakini kwa kuwa hawakuianzisha safari wao wenyewe kwa akili zao bali Mungu mwenyewe aliianzisha safari ndiye alikuwa anajua kuwa atawafikisha huko waendako. Unajua Mungu wakati mwingine anakuwa ametuonyesha twende sehemu Fulani, lakini inafika sehemu anaamua kutupitisha mahali Fulani ambapo akili yetu inakuwa imekoma ili tu atutazame, kwamba hivi tunaamini kuwa tutasonga mbele katika shida hiyo? Suala la tutapitaje katika shida hii huwa si kazi yetu, kazi yetu ni moja tu, kuwa tumwambie Yesu kuwa tumefika kwenye kizingiti hivyo tunahitaji afanye njia.
Wana waisreli walipovuka ile bahari ya shamu, haikuwa mwisho wa majaribu yao, bali ulikuwa kama ndiyo mwanzo wa majaribu yao.
YOSHUA 2:18
Wana waisraeli walipovuka mto Yordani, mtumishi wa Mungu Yoshua alichagua watu wawili waliokwenda kuupeleleza mji wa Yeriko, na haikuwa kazi nyepesi kama ambavyo wengi wanafikiri na kudhani. Maana Yeriko ulikuwa mjia ambao ulikuwa umejengwa na kuzungukwa na ukuta mkubwa na kuwa na sehemu maalumu kwaajili ya kuingilia na kutokea. Kama ambavyo miji mingi ilivyokuwa katika Afrika na sehemu zingine nyingi hapa duuniani, miji ilikuwa inazungushiwa na kuta nene kwaajili ya ulinzi na sababu zingine za usalama. Tunawaona hawa watu wawili waliotumwa kwenda kuipeleleza Yeriko, wanaingia ndani ya Yeriko kupitia lango kuu sawa sawa na wageni wengine au wasafiri wengine. Wao walikuwa wageni , na wakaenda mahali ambapo wageni wengine wangekwenda kwa kawaida, aina Fulani ya hoteli au nyumba ya kulala wageni ambayo ilikuwa imejengwa juu ya mkao wa ukuta ule. Mwanamke alikuwa ndiye mwenye hoteli hiyo na alikuwa kahaba pia. Isingeonekana kuwa kitu cha ajabu kwa watu hao kwenda mahali kama hapo, maana hii ilikuwa ni desturi ya watu wasiomcha Mungu, hata kama ilivyo mpaka leo hii.
Lakini watu wengine waliwaona wale wapelelezi na kufahamu kuwa ya kuwa walikuwa wageni. Kwahiyo mfalme akapewa taarifa za ujio na uwepo wa wageni hao, na akaamua kutuma askari ili kuwa kamata watu hao wawili. Na uwe na uhakika kabisa kuwa kipindi hicho pia kulikuwa na kusambaa kwa taarifa mbalimbali hasa za kivita kati ya falme mbali mbali, hivyo Yeriko walifahamu kwamba waisreli walikuwa karibu sana , upande wa pili wa mto. Na kutokana na yale ambayo yule mwanamke kahaba alisema baadaye, watu vilevile walikuwa wamekwisha kusikia kuhusu ule ushindi wa ajabu na wa namna yake ambao Mungu alikuwa amewafanyia wana waisraeli. Lakini yule mwanamke kahaba alikuwa na Imani na kufikiri moyoni mwake kuwa hawa watu kweli wametoka kwa Mungu.
Tunamuona huyu mwanamke kahaba alikuwa na sifa mbaya sana;
Kwanza alikuwa ni kahaba
Pili alikuwa muongo
Na Biblia iko wazi kabisa na imetaja haya yote, na Neno la Mungu haliungi mkono dhambi ya aina yeyote katika mazingira yeyote. Dhambi ni dhambi tu, haijalishi imetendwa katika mazingira yepi au katika wakati gani au kwa madhumuni gani, bado Neno la Mungu litasimama palepale. Agano la kale lilikuwa na sharia kali dhidi ya matendo machafu ikiwemo uongo ( Walawi 19:11), lakini utakumbuka Rahabu alikuwa mwanamke au mtu wa mataifa, kwahiyo alikuwa mpagani. Dini yake haikuwa na masharti kwaajili ya kuishi maisha matakatifu. Yeye alikuwa anafanya kile kilichokuwa desturi kwake. Lakini Mungu aliona ndani sana ya moyo wake, shauku ya kutaka kuijua njia ya kweli na yenye uzima wa milele. Ni kweli kabisa kuwa hatuwezi kutazamia mwenye dhambi kuwa mwenye haki kabla hajaokoka, wakati mwingine hatuwatii moyo watu hawa waovu kwenda kanisani kwa vile tuna hofu kwamba hawatampendeza Mungu, nawakati mwingine watu watatutazama vipi sisi wakutuona tukiwa na hawa watu. Lakini mkumbuke Yesu mwenyewe(LUKA 5:31), lipokuwa akiwajibu wale Mafarisayo, kwamba wasio wagonjwa hawahitaji tabibu. Kwa hiyo kukaa na watu hawa kwaajili ya lengo la kuwasaidia kiroho siyo jambo baya. Tuwalete makanisani na wlisikie Neno la Mungu kasha watatubu na kubadilika. Biblia na Neno la Mungu haliungi kono matendo ya Rahabu hata kidogo. Rahabu aliwaambia wale wapelelezi kwamba yeyey alikuwa anaamini kwamba Mungu wa Israeli angewapa nchi ile. Kwa kweli watu wote wa Yeriko walikuwa na hofu sana. Maana walikuwa wamesikia kuhusu jinsi ambavyo Mungu alikuwa amewatengenezea njia katikati ya bahari, na kuwavusha mto Yordani, pia jinsi Mungu alivyowapa ushindi juu ya Sihoni na Ogu. Rahabu naye alikuwa amesikia habari za wana waisreli kuhusu uweza na mkono wa Mungu ambavyo ulikuwa ukijidhihirisha juu yao.
Pamoja na hofu kubwa aliyokuwa nayo Rahabu, bado alikuwa tayari kumpa maisha Mungu wa Israeli, dini yake yeye mwenyewe isingetosha , japo alikuwa dini hiyo ilikuwa na miungu wengi tu, lakini Mungu huyu wa Israeli alikuwa mkuu sana na Zaidi ya miungu mingine. Yeye alikiri hivyo, na hilo ndilo lililomletea wokovu wake. Watu wengine katika Yeriko walikuwa na ufahamu huo huo lakini hawakutaka kumkiri na kumgeukia Mungu wa Israeli na hawakuhitaji msaada wake. Wowote wale ambao wangemkiri Mungu wa Israeli wangeokolewa.
Rahabu aliwaomba wapelelezi wamhurumie kama malipo kwaajili ya kuwahifadhi, na wle wapelelezi waliahidi kuwa angeokolewa wakati ambapo Mungu anewapa mji huo wa Yeriko. Yeye aliwasaidia sana, aliwapitisha dirishani kwa njia ya kamba , wakatokea nje ya ule ukuta na wakaenda zao salama. Watu wale walimpa Uzi au kamba nyekundu ili aitundike kwenyedirisha lilelile. Hii ingekuwa ni ALAMA kwao kwamba mtu yeyote ambaye alikuwa katika nyumba ile angeokolewa kama majeshi ya Israeli yangekwenda kuupiga mji wa Yeriko. Lakini Rahabu na jamaa yake wangekuwa salama kama wangebakia katika ile nyumba yake iliyo na uzi au kamba nyekundu. Hivyo kama ingetokea Rahabu akatoka nje ya nyumba yake ambayo ilikuwa na uzi mwekundu lazima naye angeuawa.
Huu uzi mwekundu unazungumzia kuhusu wokovu wa Mungu kupitia damu ya Yesu kristo wa Nazareti. Israeli walikuwa wameokolewa katika misri kwa kutia damu au kuipaka juu ya miimo ya milango wakati malaika wa kifo alipopita katika nchi ya kukaa kwao. Leo sisi tunaokolewa kwa damu ya yesu , na hakuna wokovu katika chochote kingine. Sisi tunaokolewa wakati tunapobakia chini ya ulinzi wa damu. Ikiwa tutaondoka humo na kwenda kuangalia ulimwengu wa dhambi , basi hatuna ulinzi huo tena. Wale wapelelezi wawili walijificha wao wenyewe katika mawe walipopata nafasi ya kurudi kwa watu wao. Huko watatoa taarifa kwa Yoshua kwamba Mungu alikuwa amekwisha kuwapa mji huo. Hii ilikuwa ni kwa Imani tu!
Mungu akubariki sana.

Sunday, April 23, 2017
TUNAWALETEA MFULULIZO WA MAFUNDISHO WA YA NENO LA MUNGU
Tunawaletea mfululizo wa mafundisho ya Neno la Mungu kila siku, jitahidi ku-share na wenzio ili ujumbe huu uwafikie watu wengi na Mungu wa Mbinguni atakubariki sana. Tembelea ukurasa wa facebook uitwao "MUNGU utabaki kuwa MUNGU Ministry", Twitter @drayubu2, Instagram dr-ayubu
Friday, March 17, 2017
JINSI AMBAVYO MUNGU AMEWAFUNGUA WALIOKUWA VIFUNGONI, NA KUWAPONYA WALE WALIOKUWA WAMEFUNGWA NA NGUVU ZA GIZA, WALETE WAGONJWA NA WALIO NA SHIDA MBALI MBALI
Mambo yalikuwa hivi, Yesu akaamua kuwafungua watu waliokuwa wamefungwa na kuwaponya udhaifu wa kila aina, wengine ambao wamefanyiwa maagano na wazazi wao, na maagano yakaendelea kutembea katika vizazi vyao, amesema leo atawafungua watu wengi zaidi ya vile alivyofanya, jana, juzi hata siku za zamani zile.
Tuesday, March 14, 2017
MKUTANO MKUBWA WA INJILI, LIKUYUFUSI SONGEA, WALETE WAGONJWA NA WENYE SHIDA MBALIMBALI NA YESU ATAKWENDA KUWAPONYA, ULIKOSA ZINGINE LAKINI HII SIYO YA KUKOSA: NI TAREHE 16-19/03/2017
CASFETA TAYOMI-CHUO KIKUU CHA UDAKTARI PERAMIHO WANAKULETEA MKUTANO MKUBWA WA INJILI WA AINA YAKE AMBAO UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE: 16-19/03/2017 KUANZIA SAA 9:00 ALASIRI-12:00 JIONI
MAHALI: LIKUYUFUSI SONGEA KARIBU NA BOARDER YA TANZANIA NA MSUMBIJI, NI SIKU NNE ZA UPONYAJI NA MIUJIZA.
WALETE WAGONJWA NA WATU WENYE SHIDA MABALIMBALI NA BWANA YESU ATAKWENDA KUWAPONYA.
YOHANA 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.+"
NB: WAIMBAJI MBALI MBALI WATAKUWEPO NA WATAIMBA

Saturday, February 18, 2017
JOINT MASS KUBWA ILIYOANDALIWA NA CASFETA TAYOMI - AJUCO PERAMIHO MEDICAL CAMPUS
CASFETA TAYOMI-AJUCO PERAMIHO MEDICAL CAMPUS Inawatangazia watu wote kuwa imeandaa ibaada ya Neno la Mungu,maombi, kusifu na kuabudu tarehe 19/02/2017 kuanzia saa 9:00am-13:00pm itakayofanyika katika chuo kikuu cha uganga (udaktari) Peramiho, kilometa chache kutoka hospitali ya rufaa ya mtakatifu Yosefu.
Mafundisho ya kukutia moyo mtu wa Mungu yatakuwepo, wapo walimu wazuri ambao Bwana amewaleta kwaajili yako,
HII SIYO YA KUKOSA HATA KIDOGO. WEWE MWANAFUNZI USIKOSE , UTAFUNDISHWA MAMBO MENGI KUHUSU ELIMU YAKO.
KWAYA YA CASFETA TAOMI WATAIMBA NA WAIMBAJI BINAFSI WATAKUWEPO.
WATU WOTE MNAKARIBISHWA;
WALETE WATU WOTE WENYE SHIDA MBALI MBALI NA YESU ATAWAFUNGUA:

MAPAMBANO DHIDI YA MATUMIZI NA KUUZWA KWA MADAWA YA KULEVYA NI JAMBO LA MSINGI SANA, LAKINI........
Bwana YESU asifiwe sana watu wa Mungu!
Naitwa Ev Dr. Ayubu Mathias Kwandikwa, kutoka chuo kikuu cha Askofu mkuu Yakobo (Archbishop Jamaes university College) chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Agustino, nimeokoka na ninampenda Yesu na ninamtumikia katika kazi yake kwenye eneo la uijnilisti..
Ninaunga mkono jitihada za serikali katika kupamba na suala la uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, niwapongeze viongozi mbalimbali ambao wameamua kwa dhati kabisa kutaka kulitokomeza suala hili.
Lakini kipo kitu kimoja ambacho serikali ningependa niwashauri, hakuna kitu kizuri kama kuanza na Mungu halafu ukamaliza na Mungu; Hatuwezi kufanikiwa vita hii kama watu hawajamjua Yesu kristo, unajua mtu akiokoka Anabadilishwa, anafanywa kuwa upya, matendo yote ambayo alikuwa nayo yasiyompendeza Mungu ni lazima yaachwe ili mtu awe amebadilika.
Lakini kama hatuwezi kumshirikisha Mungu hatuwezi pia kufanikiwa, na ndio maana anasema katika kitabu chake kitakatifu cha Biblia anasema "BWANA ASIPOULINDA MJI WAKESHAO WAKESHA BURE".
Na ndiyo maana tunaona mataifa mengi yamefanya vita dhidi ya madawa ya kulevya lakini bado wameshindwa, sasa uwe na uhakika pia kwetu kama tutaifanya hii vita bila kumshirikisha Mungu tutashindwa.
Madawa ya kulevya si kitu cha mchezo maana yana madhara makubwa kwa mtumiaji, familia yake, na hata jamii na taifa kwa ujumla.
Nawaasa vijana wote kujiepusha na uuzaji,utumiaji au kuwa katika mitandao ya aina yeyote inayohusu madawa ya kulevya.
Mungu awabariki sana.
Mawasiliano: ayubumathi@gmail.com

Sunday, December 18, 2016
TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU LILILOANDALIWA NA CASFETA AJUCO-PERAMIHO MEDICAL CAMPUS
Mwenyekiti Casfeta Ajuco-Peramiho Medical Campus
Saturday, August 20, 2016
MKUTANO WA INJILI - KIROMO BAGAMOYO TAREHE 2-4/09/2016
AYUBU MATHIAS KWANDIKWA(Hapo juu kwenye picha)
Kwa niaba ya Casfeta Bagamoyo Sekondari na CBGA Ninapenda kuwatangazia mkutano mkubwa wa injili utakao fanywa na Wanacasfeta Bagamoyo sekondari kuanzia tarehe 2-4/09/2016 Kiromo Bagamoyo, hivyo tunawakaribisha na tunaomba mchango wenu wa maombi na kwa wanachama wa CBGA manombwa kuchangia chochote kwaajili ya kuwezesha kufanyika mkutano huo na Mungu atawabariki sana.
Wednesday, August 17, 2016
MKUTANO MKUBWA WA INJILI - KATIKA KANISA LA MMPT - KATORO GEITA TRH 29/09-02/10/2016
Ev. Ayubu Mathias Kwandikwa ( wa pili pichani hapo juu) -mkurugenzi mtendaji-CBGA na Ev. Alberth Msengezi ( wa kwanza hapo pichani hapo juu)
Karibu katika mkutano wa injili utakaofanyika katika kanisa la MMPT KATORO GEITA kuanzia tarehe 29/09-02/10/2016 , mkutano huu utafanywa na umoja wa wanafunzi waliookoka na kumaliza shule ya sekondari Bagamoyo (CBGA) na kikundi cha "HAPA INJILI TU"
Saturday, April 23, 2016
CBGA WAWATAKIA MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA BAGAMOYO SEKONDARI
Ikiwa imebakia siku nane kabla ya kuingia kwenye MTIHANI wa taifa , CBGA wamewatakia KIDATO cha sita Bagamoyo sekondari MTIHANI mwema, akizungumza nami aliyekuwa mwenyekiti wa Casfeta Bagamoyo 2013/2014 Mh Nelson Amsi Malolo na mwenyekiti wa CBGA usiku wa Leo amesema kwa niaba ya CBGA ninapenda kuwatakia MTIHANI mwema, wamtumaini Mungu Naye atawapigania nao watanyamaza kumyaaa!
Monday, April 18, 2016
CASFETA BAGAMOYO SEKONDARI WAZINDUA ALBAM YAO YA NYIMBO ZA INJILI YENYE JINA LA "KAANANI"
CASFETA BAGAMOYO SEKONDARI hatimaye watimiza kiu ya watu wengi kwa kuzindua albam yao inayokwenda kwa jina la "KAANANI" Jana trh 17/04/2016 katika kanisa la KLPT Bagamoyo kwa Mchungaji Ndaki na kuhudhuriwa na wageni wengi huku CBGA ikiwakilishwa na yule aliyekuwa Katibu wa CASFETA wilaya ya BAGAMOYO 2014/2015 Mh Abbigail Alex Malya, mwenyekiti wa CBGA na aliyekuwa Mwenyekiti CASFETA BAGAMOYO 2013/2014 Mh Nelson Amsi Malolo amesema hiyo ni hatua kubwa sana na ameahidi kuwa wao kama CBGA hawatosita kuungamkono shughuli zinazofanywa na CASFETA BAGAMOYO katika wakati wowote.
Sunday, April 17, 2016
DR AYUBU MATHIAS AENDELEA KUANGUSHA NGOME ZA SHETANI HUKO PERAMIHO SONGEA, KUANZIA TRH 15-17/04 KTK MIKUTANO WA INJILI.
Casfeta Ajuco waendeleza mashambulizi katika mkutano wa injili huko Peramiho Songea, akizungumza na mwenyekiti wa CBGA Mh Nelson Amsi Malolo, Dr Ayubu Mathias alisema, "Tunamshukuru Mungu maana anaonekana, idadi ya watu walioikoka mpaka sasa ni watu sita (6),
Thursday, April 14, 2016
UJUE WASIFU WA DR AYUBU MATHIAS KWANDIKWA MKURUGENZI MTENDAJI CBGA, HAPA INJILI TU NA INJILI KWA WATU WOTE
Huyu ndiye Dr Ayubu Mathias Kwandikwa Mkurugenzi wa "injili kwa watu wote" na mwanzilishi wa "HAPA INJILI TU" , wasifu wake ni Daktari , amesoma shule ya msingi Lutozo-Katoro Mkoani Geita, shule ya Sekondari Katoro (2009-2012) na Bagamoyo high school (2013-2015), Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino tawi la Songea - kitivoo cha udaktari-Doctor of Medicine(2015-2020).
Tuesday, March 29, 2016
Saturday, March 26, 2016
BAGAMOYO SEKONDARI WAENDELEA NA USHUHUDIAJI WA NYUMBA KWA NYUMBA HUKO BAGAMOYO.
Akizungumza na Dr Ayubu Mathias, Mh Nelson Amsi Malolo ambaye ni mwenyekiti wa CBGA na aliye kuwa mwenyekiti wa CASFETA BAGAMOYO 2013/2014 alisema mkutano ulianza vizuri na kwa sasa wanaendelea vizuri, kikubwa wanahitaji maombi yetu.
Wednesday, March 23, 2016
MHESHIMIWA NELSON AMSI MALOLO KUHIMIZA NA KUFUATILIA MICHANGO YA CBGA KUWWZESHA MKUTANO UNAOFANYWA NA CASFETA BAGAMOYO SEKONDARI
Aliyekuwa mwenyekiti Wa CASFETA na mwenyekiti wa CBGA Mh Nelson Amsi Malolo ameanza rasmi kukusanya michango kwaajili ya mkutano injili utakaofanyika katika kanisa la FPCT Bagamoyo hapo tarehe 25/03-27/03/2016 , hivyo amewasihi na kuwa kumbusha wana CBGA waliopo katika vyuo mbali mbali hapa nchini , nakuongezea kusema wanajukumu la kusaidia na kuunga mkono jitihada hizo zinazo fanywa na CASFETA BAGAMOYO Sekondari! Hata kwa upande mwingine Dr Ayubu Mathias Naye alichangia kusema niwajibu wetu kama CBGA kuunga na kuchangia katika kila shughuli zinazofanywa na CASFETA BAGAMOYO sekondari.
Dr Ayubu Mathias, Alberth Msengezi , Dr Meshaki Anacleth , Dr Nemes Makanza na Zachariah Jonathan, kuanzisha harambee ya kumkaanga shetani
Dr Ayubu Mathias (pichani hapo juu) pamoja na wenzie wamedhamilia kufanya operation kubwa ya injili kwa kauli mbiu ya "HAPA INJILI TU" kanda ya ziwa kuanzia mwezi wa Tisa mwaka huu.
Tuesday, March 8, 2016
KARIBU SANA KATIKA HII BLOG YANGU MPYA, AMBAYO INAHUSIKA NA NENO LA MUNGU:
Blog hii sawa sawa na jina lake kuwa " HAPA INJILI TU" , ni baada ya kuona wengine wanasema hapa kazi tu, lakini sisi tulio wana wa MUNGU lazima tuseme hapa kwaajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu. Hawa wanataka magari , na Hawa wanataja Mali sisi tunalitaja jina la YESU, mtaifahamu kweli NATO kweli itawaweka nuru, YESU ndiye njia ya kweli na uzima, MTU haji kwa baba ila kwa njia ya YESU:
Subscribe to:
Posts (Atom)